|
Katika mwaka wa 1995 mwanzilishi Rafael de la Rubia alilijulisha “Dunia Bila Vita” (DBV) katika jukwaa la kimataifa kwa "Mkutano Wazi na Utu” katika chuo kikuu cha Santiago nchini Chile, mkutano ambao ulihudhuriwa na wajumbe 50 kutoka nchi tofauti.
Kutokea hapo, DBV imekuwa ikifanya mambo tofauti katika nchi tofauti bara zote. Mwaka uliopita, jitihada iliwekwa katika kampeni ya kusitisha silaha za kinuklia.
DBV imechukua mwelekeo wake kutoka kwa falsafa ya Utu Kwa Wote na kanuni za walioitangulisha ambao waliamini uwezekano wa kujenga dunia ambayo haitakuwa na vurugu.
DBV inapendekeza na kudumisha “Katiba ya Utu” ambacho kiini chake ni:
- Kushtumu vurugu ya kimwili, ambayo inadhihirishwa sana kupitia vita, pamoja na aina zote za vurugu: kiuchumi, kirangi, kidini na kijinsia.
- Kudhihirisha uhuru wa kifikira na utofauti wa kidini kwa kila binadamu.
- Uendelezaji wa sayansi na ujuzi ambao unaboresha maisha.
- Kufahamu utofauti wa watu, kabila, rangi na utamaduni kwote duniani.
- Kudhihirisha usawa wa binadamu wote.
- Kutilia maanani kuwa mwanadamu ndiye kiini cha vyote vya dhamana.
Inapendekeza kwamba binadamu hawataki vita lakini hawaamini yakwamba vita hivi vinawezwa kusitishwa. Hivyo basi, inaamini ya kuwa kuna uwezo wa kubadili fikira hizo ili watu wajue kuwa vita vinaweza kusitishwa kwa uhakika.
Kuelewa maana ya historia kuwa:
- Kung’ang’ana kuondoa maumivu na mateso kwa watu kibinafsi na kwa ujumla ili wawe na maisha yenye furaha na uhuru.
- Mvutano ambao umedumu miongo mingi ukitarajia kubadilisha mazingara yalivyo sasa kuwa mazingara ambayo yananawirisha maisha na kuleta maendeleo.
- Kila ambapo vita vimesitishwa, utu utauacha historia nyuma na kuchukua hatua kubwa katika mwelekeo wa kuzinduka kwa binadamu.
Katika kila nchi, jiji na jumuiya, DBV imewakilishwa na vikundi ambavyo vinaamini umuhimu wa kupunguzwa kwa silaha na kutokana na lengo hili, vinapanga na kuendeleza vitenzi vyao vyenyewe.
Licha ya hayo, DBV hudumisha katika jukwaa la kimataifa kampeni zifuatazo: Amani kwa Ulaya, Ulaya bila silaha za nuklia, Mediterranean bila silaha za kinuklia, Marekani ya Kirumi bila vita.
|