Siku ya Alhamisi, tarehe 02 wa mwezi wa Septemba, 2010 Bookmark and Share
Kiswahili | Available languages

Habari kuhusu maendeleo ya Maandamano ya Dunia

March Day 93 !
Oktoba 2, 2009
Januari 2, 2010


PUNTA DE VACAS 2010 - Useful Information



Maandamano ya Dunia yataanza New Zealand siku ya Oktoba 2, 2009, siku ya kuzaliwa kwa Gandhi, iliyoarifiwa “Siku ya Kimataifa ya Kupinga Vurugu” na Umoja wa Mataifa. Itakunjwa jamvi katika milima ya Andes (Punta de Vacas, Aconcagua, Argentina) Januari 2, 2010. Maandamano haya yatadumu siku 90 days, miezi tatu mirefu ya kusafiri. Yatapitia misimu yote na kwenye anga za kila nui, kutoka kaskazi na jangwa hadi kwa baridi ya Siberia. Sehemu ya safari itakayopitia Marekani na Bara Hindi ndiyo itakayokua ndefu zaidi, takriban mwezi moja. Watu mia moja wateule kutoka kwa kila asili ndio watakaoimaliza safari hiyo.


Sababu

Kwa sababu tunaweza kusitisha njaa kwa asilimia 10 ya hela itumikayo kwa silaha. Fikiri jinsi maisha yangekuwa kama asilimia 30-50 ya bajeti ya silaha ingetumika kuboresha maisha ya binadamu badala ya kutumika kusababisha uharibifu.

Kwa sababu kusitisha vita na vurugu inamaanisha kuwacha historia ya binadamu nyuma na kuchukua hatua kubwa katika uendelezaji wa asili zote za binadamu.

Kwa sababu tunaambatana na sauti za vizazi vilivyotutangulia ambavyo viliteseka kwa sababu ya vita. Mwangwi wa sauti zao bado unasikika duniani wakati ambapo vita vinavyoacha kumbukumbu ya kifo, waliopotea, vilema na waliolazimishwa kuhama makwao.

Kwa sababu “dunia bila vita” ni taswira ambayo inazipa matumaini siku za usoni na itafutayo jinsi ambavyo kunaweza kuwa na nususi pembe zote za dunia ili vurugu ipishe mazungumzo.   

Wakati wa sauti za wasio na sauti kusikika ni sasa! Kutokana na mahitaji ya dharura, mamilioni ya watu wanalilia kusitishwa kwa vita na vurugu.

Tunaweza kutenda haya yote kwa kuunganisha kani zote za amani na zile ambazo zinapinga vurugu duniani kote.

Wakati upi


Maandamano ya Dunia yataanza New Zealand siku ya Oktoba 2, 2009, siku ya kuzaliwa kwa Gandhi, iliyoarifiwa “Siku ya Kimataifa ya Kupinga Vurugu” na Umoja wa Mataifa. Itakunjwa jamvi katika milima ya Andes (Punta de Vacas, Aconcagua, Argentina) Januari 2, 2010.

Maandamano haya yatadumu siku 90 days, miezi tatu mirefu ya kusafiri. Itapitia misimu yote na kwenye anga za kila nui, kutoka kaskazi na jangwa hadi kwa baridi ya Siberia.

Nani wahusika

Maandamano haya yalianzishwa na “Dunia Bila Vita” - jumuiya ya kimataifa iliyozinduliwa na kikundi cha Harakati za Utu - ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa miaka 15 katika uwanja wa amani na kusitisha vurugu.

Maandamano haya lakini yataundwa na kufinyangwa na kila mtu. Ni wazi kwa mtu yeyote, jumuiya yoyote, vikundi, makundi ya siasa au biashara na kadhalika, ambayo yanaamini mambo sawa; mradi huu sio kitu ambacho kimefungwa. Badala yake, ni safari ambayo itaendelezwa haba kwa haba kila ambapo miradi tofauti ya watu tofauti itachangia.

Hiyo ndio maana huu ni mwaliko kwa yeyote na wote na kila mtu anaweza kushiriki. Kwa hivyo, mahali popote ambapo maandamano haya yataenda, wenyeji wanaweza kuchangia kwa kutenda vitenzi vya kila aina.  Kuna nafasi ya kila kitu ambacho mtu aweza kufikiria.

Namna ya kushiriki ni nyingi na tofauti, kama vile kushiriki kwenye maandamano yenyewe kupitia mtandao wa internet.

Haya ni maandamano ya kila mtu na ni matarajio kuwa yatafikia watu wa kila aina. Kwa hii sababu, tunawaimiza wanahabari kutangaza habari ya hii safari ya ulimwengu kueneza amani nu kusitisha vurugu.

Itayofanyika ni nini


Katika kila jiji ambayo haya maandamano yatapitia, wanajiji na vikundi wataandaa vikao, mikutano, sherehe na matukio (spoti, utamaduni, matukio yenye bashasha, musiki, sanaa, masomo na kadhalika), ambayo yatategemea na ujuzi wao.

Kwa wakati huu, mamia ya miradi tayari yashaanzishwa na watu pamoja na jumuiya tofauti. 

Lengo na Shabaha


Kushtumu hali hatari ya dunia inayotuelekeza aste aste katika upendo wa vita vya kinuklia ambayo yatasababisha baa katika historia ya binadamu.

Kuwapa sauti wanadunia wanaotaka amani. Ingawa sehemu kubwa ya watu ulimwenguni unapinga kuweka kwa hazina ya silaha na nchi tofauti, hamna ishara moja ionyeshayo azimio lao. Badala yake, tumewaacha watu wachache kutunyanyasa na kutuacha sisi kuumia na matokeo. Wakati umefika wa kusimama pamoja ili kuonyesha msimamo wetu. Ungana na halaiki ya watu kutuma ishara wazi, na sauti yako ni lazima itasikika!

Kuafikia: Kuondolewa kwa silaha za kinuklia, kundolewa kwa majeshi ambayo yameshambulia maeneo ya nchi nyingine, uendelezaji na usawazishaji katika kupunguza silaha za kisasa, kutia sahihi mkataba wa kutovamiana miongoni mwa mataifa na kukataliwa kwa vita kama njia ya kutafuta suluhu.

Kufichua aina tofauti za vurugu (kiuchumi, kirangi, kijinsia, kidini….) ambayo yamefichika au kusitirishwa na wanaoziendeleza; na kutafuta njia ambayo wale ambao wanateseka kusikika.

Kuwazindua watu – kama ilivyotendeka na suala la mazingara – juu ya umuhimu wa kushtumu aina zote za vurugu na kuleta amani.


www.theworldmarch.org ®2010 | Last change: 00:46 - 18/06/2010 (UTC/GMT) | Resolution : 1024/768 | top
Login User | Privacy | Sitemap | Sponsors | Gadgets Shop