Maandamano ya Dunia kwa Tarakimu:
Mabara: 6 Nchi: 90 Umbali: Maili 99,419 (kilomita 160,000) Muda: Siku 90
Usafiri: Safari 40 kwa gari moshi (ikiwemo kuvuka Saiberia kupitia nchi kavu). Safari 100 kupitia nchi kavu (magari ya 4-wheel drive, mabasi, motokaa, baiskeli n.k.) zikiwemo baadhi ya vijisehemu kutoka Paris hadi Dakar na kutoka Marekani Kaskazini hadi Marekani Kusini kupitia milima ya Andes. Safari 14 kwa ndege. Safari 25 kupitia baharini (meli, majahazi, mitumbwi n.k.)
Hali ya anga: Maandamano yatapitia kwenye anga za kila nui, kutoka sehemu tulivu hadi kwa zenye joto. Yatapitia hali ya anga yenye mvua wakati wa baridi na jua kali wakati wa kiangazi, ile ambayo huwa na mvua mwakani,ile yenye baridi kali na mvua, hadi kwa sehemu zilizo na barafu kwa ajili ya baridi. Maandamano pia yatapitia Siberia kupitia jangwa la Atacama hadi bara la Antarctica. Misimu: Katika siku 90, maandamano yatapitia misimu yote minne ya mwaka.
Muinuko: wakati wa safari, maandamano yatakwea hadi kwenye miinuko zaidi ya futi 16,400 (Mita 5,000) Timu: wahusika 50. Mipaka itakayovukwa: 160 Taasisi saidizi: 500 Taasisi zilizoungana nasi: 3,000 Ziara kwa serikali tofauti na kwa manaibu wa kisiasa: 100 Taasisi za kidini: 25
Wahusika wa ziara: milioni 1 Wahusika watakaoshiriki kupitia kichakato: milioni 10
|